Marioo aingia studio na Bien

Marioo aingia studio na Bien

Baada ya mwanamuziki Marioo kutua nchini Kenya na kupokelewa kwa shangwe, ameingia studio na msanii Bien.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Marioo amechapisha picha akiwa na msanii huyo, ambapo picha za wawili hao wanawaonesha wakiwa studio.

Hii itakuwa ‘kolabo’ ya kwanza kwa Marioo kuifanya na msanii huyo wa Kenya. Kwa upande wa Bien amewahi kutoa ngoma na wasanii wa Tanzania kama Darasa, Joh Makini, Harmonize na wengineo.

Ikumbukwe Marioo alitua nchini Kenya jana siku kwa lengo la kutumbuiza katika show ya ‘Turn Up The Heat’ inayotarajiwa kufanyika nchini humo kuanzia Septemba 18 hadi 22 mwaka huu.

Hata hivyo baada ya kutua Kenya Marioo alikabidhiwa bendera ya nchi hiyo pamoja na kupewa jukumu la kuutangaza muziki wa Kenya katika mataifa mbalimbali.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags