Mark Rubani mdogo zaidi kurusha ndege

Mark Rubani mdogo zaidi kurusha ndege

Na Habiba Mohammed

Weeeuuuweee! Kuna kale kamsemo kanasema" umri ni namba muhimu kupambania ndoto zako" Sasa wenzangu na mie misemo kama hii huwa hatuchukulii uzitoo ,tunajidharau na kuyapa kipaombele mawazo ya watu.

Basii bhana unaambiwa kijana mwenye umri wa miaka 17 anayefahamika kwa jina la Mack Rutherford mzaliwa wa Ujerumani mwenye asili ya Ubelgiji ndo mtu mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kuendesha ndege peke yake kwa mujibu wa Guinea Book or Records

Mack Rutherford alifanya safari ya miezi 5 na kutua Sofia huko Bulgaria na baada ya hapo aliweza kwenda mataifa mengine 52,vilevile katika record ya Dunia Kijana huyu ndiye anayeshikiria kuwa Rubani mwenye umri mdogo kuwahi kutokea Aidha Mack Rutherford alihitimu mafunzo yake ya urubani akiwa na miaka 15.

Aiseee!kwelii udhubutu na kujiamini ni kitu muhimu katika kufikia ndoto yako ,Basii wenzangu  mie dondosha comment yako utuambie katika umri wa 13-17 ulifanya Nini kama ishara ya kupigania ndoto yako.

 

Chanzo BBC






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags