Kupitia ukurasa wake wa instagram msanii kutokea Lebo ya WCB amewashukuru mashabiki zake kwa muitikio mkubwa waliuonesha baada ya kuachia kionjo cha wimbo wake wa‘Inamana’.
"Asanteni kwa mapokezi ya wimbo wangu wa Inamana kinachonisikitisha ni kwamba nilikuwa natest mitambo tu nikapost kionjo ila nimeona ni jinsi gani mapenzi yanawatesa watu wangu" ameandika Lavalava.
Mbali na kutoa shukrani hizo lakini pia amewataka mashabiki wachague atoe ngoma za aina hiyo mfululizo au aanze na Inamana kwani nyimbo hizo zipo zaidi ya 10.
Kionjo cha wimbo wa Inamana ya Lavalava alikiachia siku mbili zilizopita kupitia mitandao yake ya kijamii na kupokelewa kwa ukubwa katika mitandao ya kijamii hasa TikTok.
Unamkubali Lavalava Wa Amapiano Au Akiimba Nyimbo Za Mapenzi?
Leave a Reply