Mayele: Mimi ndio nastahili kuwa mfungaji bora

Mayele: Mimi ndio nastahili kuwa mfungaji bora

Baada ya msimu wa Ligi kuu soka Tanzania bara 2022/2023 kumalizika huku Wachezaji Fiston Mayele wa Yanga na Saido Ntibazonkiza wa Simba SC wakilingana magoli 17 katika mbio za kuwania tuzo ya Mfungaji bora, Mayele amesema anayestahili Tuzo hiyo ni yeye.

Mayele ameyasema haya wakati akiwa LIVE kwenye Instagram yake akisherehekea Ubingwa wa Yanga baada ya kuifunga Prisons Jijini Mbeya hapo jana, mwamba huyo amefunguka na kueleza kuwa “Tushachukua Ubingwa na kiatu tena tunachukua kwa sababu mimi sina goli la penati, wataumia sana leo kwa sababu matumaini yao ilikuwa kiatu” amesema Mayele

Mijadala imekuwa mingi mitandaoni na swali kubwa ni nani atapewa tuzo hiyo ukizingatia kwamba kwenye Ligi Kuu Tanzania hakuna kanuni ya moja kwa moja inayoeleza nani atapewa tuzo ikitokea Wachezaji wamelingana magoli japo kuna baadhi ya Mataifa Wachezaji wote hupewa Tuzo mfano (England) huku Mataifa mengine yakimpa Tuzo aliyefunga goli chache za penati.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags