Mbuzi washinda kesi ya uzururaji

Mbuzi washinda kesi ya uzururaji

Kundi kubwa la mbuzi wakorofi wenye tabia ya kuzurura katikati ya mji nchini Uingereza wameachiliwa huru baada ya kushinda kesi ya uzururaji.

Mbuzi hao wa ‘Kashmir’ wamekuwa wakizurura mitaani kwa zaidi ya miaka 100 wakiwa na tabia mbovu za kula mimea na uzio wa nyumba za watu.

Wanyama hao hao wenye pembe ndefu waliingia kwenye hoteli, wakipanga foleni nje ya nyumba ya utunzaji wakati wa chakula cha jioni wakitarajia chakula na kutembelea kituo cha huduma ya chakula ya ndani.

Daily Star ililipoti kuwa, baraza la Halmashauri ya Llandudno, North Wales iliamuru mbuzi hao kuachiliwa licha ya tabia zao mbovu, likisema ni jukumu la wamiliki wa ardhi kulinda mali zao kutoka kwa mbuzi hao badala ya kuzuiliwa.

Kutokana na kusababisha maafa kwa jamii mara kadhaa wakazi wa Wales wamekuwa wakitaka kuwapiga risasi mbuzi hao ili watoweke kwenye makazi ya watu

Hata hivyo, pendekezo hilo lilikataliwa kufuatia maandamano makubwa ya umma mjini Bodlondeb. Mbuzi hao walipata umaarufu mwaka wa 2020 walipovamia mitaa iliyoachwa tupu wakati wa janga la kimataifa la COVID-19.

Zaidi ya mbuzi 200 huondoka mara kwa mara kwenye eneo la Orme mkuu na kurandaranda mitaani.

Kwa mujibu wa ripoti ya Baraza la Halmashauri, hakuna mtu au shirika lolote ambalo linawajibika kisheria kwa idadi ya mbuzi hao ambao Malkia Victoria alitoa kama zawadi kwa kiongozi wa eneo hilo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags