Mchoraji Azamat kumkabidhi Ronaldo picha ya misumari ya dhahabu

Mchoraji Azamat kumkabidhi Ronaldo picha ya misumari ya dhahabu

Msanii wa Krygystan Azamat Zhanaliev ameandaa zawadi maalumu ya sherehe ya siku ya kuzaliwa kwa ajili ya mchezaji maarufu wa soka duniani Cristiano Ronaldo maarufu kama CR7 ambayo ni siku ya tarehe 5 Februari.

Tarehe Mosi Januari, 2023, Ronaldo, aliyeanza kuchezea klabu ya soka ya Al-Nassr Saudi Arabia, alitimiza umri wa miaka 38. Iliripotiwa kuwa mkataba aliosaini na klabu hiyo katika mji mkuu wa Saudi Arabia Riyadhi ni wa thamani ya euro milioni 200.

Msanii Azamat Zhanaliev sasa anataka kutoa zawadi ya picha ya Ronaldo iliyotengenezwa kwa misumari 7777 ya dhahabu na kamba.

"Hii sio zawadi yangu tu, ni zawadi kwa niaba ya nchi yetu nzima, mashabiki wa soka," Azamat Zhanaliev aliiambia bbc
Azamat Zhanaliev anasema kuwa amekuwa akifanya kazi yake kwa miaka saba na tayari ametengeneza picha 76 za watu kwa kutumia misumari na waya.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags