Mendy: Nishafanya ngono na wanawake 10,000

Mendy: Nishafanya ngono na wanawake 10,000

Mwanasoka kutoka klabu ya Manchester City, Benjamin Mendy mwenye umri wa miaka 28 anatuhumiwa kwa kosa la kumbaka msichana mmoja mwenye umri wa miaka 28 na kumwambia msichana huyo “ni sawa, kwani ameshafanya ngono na wanawake 10,000”.

Mendy anatuhumiwa kumshambulia mwanamke huyo, wakiwa kwenye jumba lake la kifahari huko Mottram St Andrew, Cheshire, Oktoba 2020.

Aidha anatuhumiwa kwa jaribio la kumbaka msichana mwingine, mwenye umri wa miaka 29 ambaye pia alimshambulia nyumbani kwake miaka miwili iliyopita.

Baada ya kusomewa mashtaka yote mawili katika Mahakama ya Chester na Jaji Stephen Everett, mwanasoka huyo alikanusha kuwa hakufanya makosa hayo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags