Meneja: Hali Ya Zee Cute Bado Sio Nzuri

Meneja: Hali Ya Zee Cute Bado Sio Nzuri

Meneja wa msanii wa Bongo Fleva, Zee Cute, Baraka Frank, amethibitisha msanii huyo kuanza matibabu maalum kutokana na changamoto ya Afya ya Akili iliyoanza kumsumbua mwezi Mei, 2025.

Akizungumza na Mwananchi leo Juni 19, 2025, Meneja huyo amesema hali ya Zee Cute bado sio nzuri lakini tayari ameanza matibabu ikiwa leo ni siku ya tano tangu aanze kupata uangalizi maalumu wa daktari.

“Tunamshukuru Mungu matibabu yameanza, anasiku kama ya tano tangu ameanza kupatiwa matibabu ya changamoto anayopitia, naweza kusema hali niyakawaida nasisi tunasubiri majibu kwa mtu anayemuhudumia, bado hali yake haiko vizuri naweza kuthibitisha hilo, hali ya msanii haiko vizuri,”amesema

Amesema dalili za changamoto hiyo alianza kuziona mwezi Mei, 2025, ambapo hali ilibadilika ghafla wakati wanashuti moja ya video za msanii huyo.

“Hii hali nimeanza kuiona kuanzia katikati ya mwezi watano kunasiku tulikuwa location tunashuti hatukumaliza nikaanza kujiuliza kunachangamoto zilitokea, huyu mwenzetu vipi mbona hatumuelewi kwaiyo nilianza kuhisi hali mbaya pale lakini sikuitilia manani kwahiyo baada ya mambo kutokea hivi ndio nakagundua huwenda tungegundua mapema isingefikia huku,” amesema Baraka.

Meneja huyo amedai kuwa mwanzoni Zee Cute alianza kuonesha dalili mbaya ambazo sio sawa kuzitaja kwasasa mpaka pale mwenyewe atakapohiaji kuweka wazi.

"Kiukweli nisingependa kuzizungumza lakini ni dalili ambazo sio nzuri kuzizungumza kwenye jamii kwa sababu bado yupo kwenye matibabu na hata akimaliza matibabu hayo akafahamu nilielezea hazijakaa sawa nadhani hata kwenye jamii hatuwezi kuzingumza, lakini hazijakaa sawa na haziko sawa, ni bora kuutunza utu wake kuliko kuutweza" amesema Baraka.

Hata hivyo, Baraka amekiri timu ya msanii huyo walichelewa kugundua tatizo hilo kitu kilichopelekea hali ya Zee kuwa mbaya zaidi, pia ametoa rai kwa watu wasichukulie poa wanapoona ndugu au rafiki anapitia tatizo hilo.

“Iko hivi unajua watu wengi hatuna elimu na haya mambo, ndio maana nikasema ukiona mtu anasema hayuko sawa tusichukulie poa, unajua mwanzaoni wakati inatokea tuliona nikama vitu vya kawaida na kuna muda alikuwa anatamani kuzungumza lakini alikuwa anaona hakuna mtu anaemsikiliza, sisi tulichelewa kumjua mwenzetu nini anapitia, nikweli tumechelewa nakiri kweli, kwasababu hatukuwahi kujua hili tatizo linaanzaje,” amesema Baraka

Amesema hali ya ugonjwa huo imeathiri kwa kiasi kikubwa ufanyaji wa kazi zake jambo ambalo limepelekea shughuli zao nyingi za kimuziki kusimama.

“Kiukweli imeathiri pakubwa kwa sababu naweza nikasema kwamba kuanzia mwezi watano katikati mpaka sasa kunavitu vingi vilikwama hata utendaji wakazi ulipungua yaani kuna vitu vingi vilipotea na kuondoka kwenye mipango yetu, kwahiyo kwenye utendaji vitu havijakaa sawa vingi vimetoka kwenye utaratibu, sisi kama uongozi tumewekeza nguvu kubwa kwenye matibabu kuhakikisha anarejea kwenye utimamu wa mwili na akili"

Pia, ametoa rai kuhusu baadhi ya mastaa ambao wanazungumzia swala hilo tofauti akihusisha kauli ya muongozaji wa video za za muziki nchini, Hanscana aliyoitoa hivi karibuni kuhusu kutofautisha Umasikini, Afya ya Akili, Depression na msongo wa mawazo.

“Labda mimi kwanza nisemi kitu hiki changamoto yoyote ile ambayo mwanadamu anapitia inaweza kupelekea kupata msongo wa mawazo, kwasababu watu wote wamepewa uwezo binafsi wakuhimili vitu, mtu anaweza kuwa na changamoto akaweza kuihimili, mwingine asiweze, anachokizungumza.

Hanscana anauelewa wake lakini kwenye Afya ya Akili kwamba tusichukulie poa wala kufanya masihara kabisa kwani mtu mwenye changamoto hiyo anaweza kukudhuru wewe au akajidhuru mwenyewe, kwasababu msongo wa mawazo unakutoa kwenye dunia ya kawaida na unakuwa kwenye dunia yako" Amesema

Zee Cute ni mmoja wa wasanii wa Bongo Fleva ambae anafanya poa kwasasa akitamba na kazi zake kama Nakuja, Nikupe, Huku, Boyfriend akifanikiwa kushirikiana na wasanii kama Hamadai, Vanillah, Ibraah, na wengine wengi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags