Moja ya wimbo ambao umekuwa ukikubalika zaidi hasa kipindi cha huzuni ni ‘See You Again’ uliyoimbwa na mwanamuziki Wiz Khalifa akimshirikiana na Charlie Puth.
Wimbo huo uliachiwa rasmi Machi 10,2015 huku ukitumika katika filamu Furious 7 kama heshima kwa marehemu mwigizaji Paul Walker, ambaye alifariki dunia mwaka 2013 katika ajali ya gari.
Baada ya kifo cha Walker, waandaaji wa filamu walihitaji wimbo wenye hisia nzito za kuaga na kushukuru urafiki ambapo rafiki wa karibu wa marehemu mwigizaji huyo Charlie Puth aliamua kuandika wimbo huo huku Wiz akiongezea mistari ya Rap.
‘See You Again’ unatajwa kuwa wimbo uliofanya filamu ya Furious 7 kuwa moja ya filamu zenye mafanikio makubwa na za kihisia sana katika historia .
Mafanikio ya ngoma hiyo ndani ya miaka 10
Wimbo huo ulifanikiwa kupata mafanikio mbalimbali ambapo ulishika nafasi ya kwanza katika chati za Billboard Hot 100 kwa wiki 12 mfululizo vile vile uliongoza chati za muziki zaidi ya nchi 30, ikiwemo Uingereza, Australia, Canada, na Ujerumani.
Aidha ulivunja rekodi kwa kuwa wimbo uliosikilizwa zaidi ndani ya siku moja katika mtandao wa Spotify mwaka 2015. Ulifikisha watazamaji zaidi ya bilioni 1 katika mtandao wa YouTube ndani ya miezi minne.
Huku mwaka 2017 ukiweka rekodi ya kuwa wimbo wenye watazamaji wengi zaidi kwenye YouTube kwa muda mfupi kabla ya rekodi hiyo kuchukulowa na wimbo wa Despacito ulioimbwa na Luis Fonsi.
Tuzo
Mbali na kupata mafanikio hayo lakini pia wimbo huo uliwahi kunyakuwa tuzo kama Billboard Music Awards, Teen Choice Awards, na Critics' Choice Awards huku mwaka 2016 ukichaguliwa kuwania Grammy katika vipengele vitatu ikiwemo Song of the Year, Best Pop Duo/Group Performance na Best Song Written for Visual Media.
Hata hivyo ulifanikiwa kuuza zaidi ya dola milioni 20 duniani kote pamoja na kupata Platinum mara nyingi katika nchi nyingi, ikiwemo Marekani (11× Platinum), Uingereza, Australia, na Canada.
‘See You Again’ unatumika kama wimbo wa kukumbuka waliopoteza maisha huku ukiwapa faraja ndugu waombelezaji huku ukisikika mwishoni mwa filamu ya Furious 7

Leave a Reply