Mitazamo Tofauti Wasanii Kujitangazia Dau

Mitazamo Tofauti Wasanii Kujitangazia Dau

Mwandishi Wetu, Mwananchi

Miaka 12 iliyopita, msanii Naseeb Abdul 'Diamond aliwahi kueleza Bila malipo ya Sh 10 Milioni hafanyi kolabo.

 

Hiyo ilikuwa ni Juni 6, 2012, wakati huo watu wengi walimbeza na wengine kumuona anaringa wakiamini hataki kufanya kolabo na wasanii wengine.

 

Leo hii Diamond ni miongoni mwa mwanamuziki Watanzania wanaoingiza pesa nyingi kupitia kipaji chake cha muziki.

 

Novemba 26, 2023 muimbaji wa Bongo Fleva, Jay Melody alisema alisema hafanyi shoo chini ya Sh 10milioni anapiga mkwanja mrefu zaidi.

 

Hivi karibuni video vixen, Nai alisema bila miloni 10 hafanyi video ya msanii yoyote, labda kutoka nje ya nchi na wasanii ambao ni wakubwa.

 

 

Nyuma ya pazia ipo hivi

 

Mtayarishaji nguli wa muziki nchini, Master Jay anasema kwa Tanzani, msanii akitangaza dau kama hivyo anaonekana anaringa, jambo ambalo si sawa.

 

"Kwa wenzetu wa nje maisha ndiyo yapo hivyo, unapomfuta msanii mkubwa ni kwamba wewe ndiye unakwenda kutumia nguvu zake za kibiashara, hivyo hawezi kukubusti bure.

 

"Mfano ni Naseeb (Diamond) alivyofanya kazi na Davido, mwanamuziki huyo alimchaji pesa aliyoitaka.

 

"Itakuwa walizungumza kwamba nahitaji kiasi fulani kwa ajili ya kurekodi na kiasi fulani kwa video,".

 

Anasema ile ni biashara akitolea mfano namna Diamond alivyokuwa tofauti baada ya kufanya kazi na Davido.

 

Diamond na Davido walifaya ngoma ya My number One Remix iliyotoka mwaka 2014.

 

"Muziki ni biashara, Watanzania huwa tunaona ni kitu cha ajabu msanii akisema bila kiasi fulani hafanyi kolabo au shoo kutokana na misingi tuliyorithishwa ya Ujamaa.

 

"Lakini katika biashara hususani ya Muziki, msanii mkubwa hawezi 'kumbeba' bure aliyechini yake kwa kuwa hata yeye hati kufika hapo aliwekeza pesa nyingi.

 

Anasema, Babu Tale (Meneja wa Diamond) aliwahi kueleza namna Diamond alivyowekeza pesa nyingi kufanya kolabo na Davido, jambo ambalo lilimbadilisha Diamond baada ya kazi hiyo.

 

Babu Tale alipotafutwa na gazeti hili, aliomba atafutwe siku nyingine kwa kuwa yupo kwenye mkutano wa Chama Dodoma.

 

Mameneja wafunguka

 

Meneja wa Ibraah wa lebo ya Konde Music WorldWide, Mabruki Nyoya (Uncle Duke) anasema msanii kujitangazia dau hilo ni kuji-brand.

 

"Hii inamfanya atengeneze value (thamani yake) kibiashara, akifanya hivyo mtu anapotaka kumfuata kufanya naye kazi anakuwa anajua kabisa kwamba huyu kiasi chake lazima nisiwe chini ya milioni kadhaa," anasema.

 

Anasema pamoja na kutangaza hivyo, lakini nyuma ya kamera anaweza kufanya kazi chini ya kiwango hicho kama mkikaa mezani na kuzungumza.

 

Anasema wasanii wngi, hadi kufikia kutaja dau ni yule aliyefikia levo ya juu, anaimarisha brand yake.

 

 

Meneja wa Chino Wana Man, Esi 'Love' Mgimba anasema hadi msanii kufia levo ya kuweka dau lake wazi huwa ameona ni namna gani amewekeza hadi kufika hapo alipofika.

 

"Atakuwa ameiona thamani yake na kuona huo ni wakati wake kulingana na brand yake, sio kwenye muziki tu, hata katika biashara huwa inatokea unaweza kukuta bidhaa ni ile ile, lakini duka A utainunua kwa Sh 980 na duka jingine ukainunua kwa Sh 550," anasema Esi Love.

 

Anasema msanii hadi kutangaza dau lake kwenye kazi huwa anajua ni kwa namna gani amewekeza hadi kukuza brand yake na kufika hapo alipofika.

 

"Wengi huwa inawasadia kwa kuwa mtu akitaka kufanya kazi na msanii huyo haji kichwa kichwa, atamfuata akijua kabisa lazima niwe na kiasi fulani cha pesa ili msanii huyo afanye kazi yangu," anasema.

 

 

John Kimambo, meneja wa mwanamuziki Marioo anasema kila msanii ana namna yake ya kujibrand kutokana na namna watu wanavyomfahamu.

 

"Hivi sasa kuna wasanii wa aina tofauti tofauti, wapo wanaotengeneza maudhui mitandaoni kwa kufanya vituko na watu wakawapenda na kujulikana.

 

"Wasanii wa aina hiyo wao kusema bila milioni kadhaa hafanyi kazi, kwao hakuna impact (maana) , lakini kwa wale ambao wamejibrand kwa staili ya kuwekeza muda, pesa hii ni kawaida," anasema.

 

Anasema ili mfumo uwe uwe na maana, inategemea na msanii gani amesema kwa wakati gani na kwa misingi ipi?.

 

"Inaweza kuleta matokeo chanya au hasi kutokana na aina ya msanii aliyezungumza na brand yake ikoje," anasema.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags