Mtoto mwenye mwili wa sumaku

Mtoto mwenye mwili wa sumaku

Na Habiba Mohamed

Niajeee niajeeeeeeee!!majabu yanazidi kila siku na kama ilivyokawaida lengo nikupa habarii uhabarikee na ufurahie maana ndo jukumu letu haswa, basi bwana huko Ulaya kijana anayefahamika kwa jina la Ivan amezua gumzo baada ya kusema yuko na nguvu ya sumaku mwilini mwake

Kwa kusithibitisha Hilo kijana Ivan  akaonyesha uwezo huo kwa kunasa vitu vyenye asili ya chuma kama vijiko,sufuria na vinginevyo vinavyoweza kunasa kwenye sumaku.

Aidha Kutokana na uwezo alionao mtoto huyo uchunguzi uliofanyika ilionyesha kwamba nyakati za asubuhi mtoto huyo anauwezo wa kunasana vitu vyenye asili ya chuma vyenye kilo 25 kifuani mwake lakini  pia nyakati za mchana anaweza kunyanyua vitu vyenye kilo 18.

Aiseeeeeee walimwengu kila tukio kwetu kivutio ,basi watalii wa huko Ulaya wamevutiwa na uwezo alionao mtoto huyo na uwezo huo umemfanya kuwa maarufu duniani kote na yeye pia kujipatia kipato kwa kufanya maonyesho kupitia uwezo wa kunyanyua vitu vya chuma.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags