Mtoto wa Mfalme Dubai amtaliki mumewe Instagram

Mtoto wa Mfalme Dubai amtaliki mumewe Instagram

Binti wa mtawala wa Dubai, Sheikha Mahra Bint Mohammed Bin Rashid Al Maktoum, amempa talaka mumewe Sheikh Mana bin Mohammed bin Rashid bin Mana Al Maktoum kupitia mtandao wa Instagram.

Talaka hiyo iliyotolewa Insta imekuja miezi kadhaa baada ya wanandoa hao kupata mtoto wao wa kwanza ambaye ni wa kike.

Katika talaka hiyo ilikuwa imeandika,

“Mume wangu mpendwa, natangaza talaka yetu. Nakutaliki, nakutaliki, nakutaliki,” aliandika prince wa Dubai kwenye Instagram. Hata hivyo kabla ya talaka hiyo Sheikha alichapisha picha akiwa na mwanaye na kusindikiza na ujumbe usomekao “Sisi wawili tu,”.

Fahamu kuwa baba wa binti huyo aitwaye ni mwanasiasa na mfalme wa Kiarabu ambaye ni mtawala wa sasa wa Dubai.

Hivyo basi Sheikha ni mmoja wa watoto 26 wa mtawala huyo. Mama yake, Zoe Grigorakos anatoka Ugiriki, hivyo binti huyo ana asili ya Kiarabu na Kigiriki. Hata hivyo Mtawala huyo wa Dubai haishi na mama wa biti huyo kwani walitengana muda mrefu






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags