Mwana Fa Aitaka Cinderela Remix

Mwana Fa Aitaka Cinderela Remix

Baada ya remix ya wimbo wa ‘Yule’ kutoka kwa mkongwe wa muziki Bongo AY na Marioo kupokelewa vizuri, na sasa Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa, Michezo Mwana FA ametoa maoni yake kuhusu ngoma ya ‘Cinderela’ ya Alikiba.

Kupitia ukurasa wa X (zamani twitter) wa FA ameshare ujumbe kuwa anadhani kuna msanii anatakiwa kufanya remic ya wimbo huo.

“Kwa maoni yangu kuna mtu (msanii) anatakiwa ku’remix Cinderela” ameandika Mwana FA

Utakumbuka kuwa wimbo wa Cinderella ndiyo ngoma ambayo ilimtambulisha Alikiba kwenye muziki wa Bongo Fleva huku mwaka 2006 aliachia rasmi albumu yake ya kwanza yenye jina la ‘Cinderella’ ikiwa na nyimbo 15 ambazo zilikubalika zaidi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags