Myths kuhusu maisha ya chuo

Myths kuhusu maisha ya chuo

Hahhahaha! Make hapa kwanza ncheke, natumai ni wazima wa afya watu wangu wa nguvu, leo basi katika UniCorner tumekuja na mada konki kabisa, I hope wengi wenu itawajenga zaidi katika maisha mapya ya chuoni.

Hakuna kitu ambacho hautakisikia kuhusu hatua yoyote unayoiendea maishani na hivyo pia hata ukiwa unaenda chuo au ukiwa chuo, utasikia maneno mbalimbali. Mengi yatakuwa ya ukweli lakini pia mengine yatakuwa ya uongo na leo nitaongelea machache ya uongo ambayo utayasikia na uliambiwa na kaka yako, ndugu au rafiki.

Huu ndio uongo ambao utaambiwa na kuuskia kabla hujaanza maisha ya chuo:

  • Chuo bata

Hehehhe! hili linaongelewa sana na utaambiwa sana au hata umeanza kuamini hili ila sio bata kwamba maisha ya chuo ni rahisi, sio rahisi. Kiukweli maisha ya chuo yanastress sana, hasa mahitaji yake yanavyokuwa mengi, kwahiyo jua kubalance muda wako. Utapata muda wa kula bata ila sio kwamba maisha yako yatakuwa bata muda wote.

Na basi ukiendekeza bata wanalolisema waja basi utakuja kukumbushwa na GPA yako hapo mwisho wa muhula ndo utajua ni bata au ni kuku. Ukijua kupangilia majambo yako basi maisha ya chuo utayaona bata haswaaa.

  • Ety bila laptop, chuoni hauwezi soma

Labda niseme hivi, kuna matumizi mengi ambayo kuwa na laptop yangekusaidia, lakini asilimia 80 ya jinsi tunavyotumia laptop chuo ni kwaajili ya movie.

Wengi tulikuwa tunaitumia hivyo. Kama kweli kusoma hata smartphone unaweza kusomea na nina mifano mingi ya wanafunzi ambao walitumia smartphone tu kusomea na tumemaliza nayo fresh tuu.

Kwahiyo isikupe presha sana kama hauna uwezo wa kununua sasa, utanunua tu utakapofanikiwa kiuchumi au utakapoona umuhimu wake, usijipe presha kwasababu ya laptop, smartphone inatosha.

Angalia apps mbalimbali unazoweza kuziweka kwenye simu yako ambazo zitakufanya upate mahitaji yako yote ambayo ungeyafanya kwenye laptop; mfano WPS.

  • Kila somo liwe na daftari lake

Stori ya kweli nahisi nimemaliza chuo na madaftari manne kama sio matatu daftari moja nilitumia kuandikia masomo matatu na hii ni kutokana na soft copies ambazo unaweza kuzisoma kwenye smartphone ama laptop, muda mwingi unajikuta unatumia soft copy kuliko kuandika. So usidanganyike kuwa chuo lazima uwe na daftari la kila somo.

  • Chuoni hakuna kufeli

Uwiiiih! Najua huku shuleni tulikuwa ukifeli ndio inaonekana kama mwisho wa dunia na ndio maana supp, carry na disco havionekani kama vikubwa kwasababu havioneshi kukunyima nafasi nyingine tena kama mitihani ya NECTA. Ila usichezee elimu ya chuo kwasababu ‘kufeli’ kwake hakufanani na ulikokuzoea.

Huu ni uongo mkubwa na ukiutilia maanani ili usisome basi utakuja kujuta baadae, chuo kufeli kupo pale tu ukiwa hujitambui na kupotelea  katika msemo huo wa chuoni hakuna kufeli.

  • Usipopata mchumba chuoni huwezi pata tena

Aloooh! Nakumbuka marafiki zangu tulikuwa tunasema sisi haya mambo mengine tukiwa chuo wacha yatupite, mfano kama haya ya kuwa na mahusiano chuoni.

Ni hivi, unaenda chuo kusoma na sio kutafuta mke au mume, ukimpata tunamshukuru Mungu na usipompata sawa na statistics zinaonyesha ni asilimia chache sana ya mahusiano ya chuo ndio hufikia mpaka ndoa na hata hivyo watu hukutana sehemu mbalimbali sio lazima iwe chuoni usiwe na papara na kwenda kutafuta yasiyokupeleka.

Nikushauri tuu usijiingize katika huyu ujinga kisa tuu umesikia msemo huo au kisa tu umemuona rafiki yako ana mahusiano basi na wewe utafute wakumtafuta uwe nae, heheh rafiki yangu utachezewa sanaaa, sitaki kukuficha.

Haya haya mwanangu sana embu njoo katika mitandao yetu ya kijamii  @Mwananchiscoop na utueleze ni uongo gani ambao ulidanganywa kuhusiana na maisha ya chuo na wewe ukaukubali.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post