NDOA YA AZIZ KI NA HAMISA KUFUNGWA MUDA MCHACHE UJAO

NDOA YA AZIZ KI NA HAMISA KUFUNGWA MUDA MCHACHE UJAO

Baada ya tukio la kutoa mahari lililofanyika mapema Jana Jumamosi Februari 15,2025, hatimaye ndoa ya wawili hao inatarajiwa kifungwa leo kwenye moja ya msikiti uliyopo Mbweni.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa chaneli ambayo inarusha moja kwa moja sherehe hiyo imeeleza kuwa ndoa hiyo itafungwa msikitini na baada ya hapo bwana harusi na wapambe wake watakwenda nyumbani kwa mama Mobetto, Mbweni jijini Dar es salaam kwa ajili ya kumchukua bibi harusi.

Utakumbuka mwanamitindo Hamisa Mobetto Jumamosi, Februari 15, 2025, amelipiwa mahari  ya ng'ombe 30 na kiasi cha Sh 30 milioni na Stephanie Azizi Ki ambaye ni kiungo mshambuliaji ya Yanga.

 

Mahari hiyo imekabidhiwa na Injinia Hersi Said, kwa niaba ya baba mzazi  na wajomba wa Aziz Ki, ambapo nyota huyo wa Yanga aliongozana na baadhi ya wachezaji wenzake kama Pacome Zouzoua, Bakar Mwamnyeto, Yao Kouassi na wengine sambamba na maofisa Habari wa klabu hiyo, Ali Kamwe na Priva.

 

Baada ya kufunga ndoa lakini pia kutakuwa na sherehe nyingine ambayo itafanyika Februari 19 kwenye ukumbi wa Superdome Masaki Jijini Dar es Salaam.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags