Majadiliano yaendelea hatma ya Diddy

Majadiliano yaendelea hatma ya Diddy

Majaji wameanza majadiliano rasmi katika kesi inayomkabili rapa maarufu wa Marekani, Sean “Diddy” Combs, ambaye anakabiliwa na mashitaka ya usafirishaji wa binadamu kwa ajili ya ngono, vitendo vya kihalifu na mengineyo.

Hatua hii inakuja baada ya ushahidi kutolewa kwa zaidi ya wiki sita uliyowasilishwa na upande wa mshtakiwa huku upande wa utetezi (Diddy) ukigoma kupandisha shahidi hata mmoja.

Majadiliano hayo yalianza rasmi Juni 30,2025 baada ya mawakili wa pande zote mbili kutoa hoja zao za mwisho. Ambapo waamuzi hao watakuwa na kazi ya kuchambua ushahidi uliotolewa na mashahidi wakiwemo wafanyakazi wa zamani wa Diddy huku hukumu ikitarajiwa kutolewa wakati wowote kuanzia sasa.

Waamuzi, hao wanaume wakiwa nane na wanawake wanne ambao majina yao yamehifadhiwa kwa usalama wao, wamepewa maagizo maalumu ya kisheria kuhusu namna ya kuchambua ushahidi huo lakini pia kutoa uamuzi wa pamoja juu ya kila shtaka ili kutoa hukumu ya halali.

Diddy anakabiliwa na mashtaka ya usafirishaji wa binadamu kwa ajili ya ngono, njama ya kihalifu na usafirishaji kwa lengo la kushiriki katika ukahaba.

Hata hivyo, rapa huyo alikanusha mashtaka yote, kupitia mawakili wake, akisisitiza kuwa yeye ni mhanga wa kampeni ya kumharibia jina, na kwamba vitendo vyovyote vilivyotokea vilikuwa kwa ridhaa ya watu wote waliokuwapo. Wakili wake mkuu, Teny Geragos, alisema hakuna ushahidi wa moja kwa moja unaoweza kuthibitisha shutuma hizo.

Utakumbuka Sean "Diddy" Combs alikamatwa Septemba 16, 2024 katika hoteli ya Park Hyatt, Manhattan, New York na kupelekwa moja kwa moja katika gereza la Metropolitan huko Brooklyn. Kesi yake ilianza kuzikilizwa Mei 5,2025. Huku mashahidi mbalimbali wakitoa ushahidi akiwemo rapa Kid Cudi, Cassie, Jane, Mama mzazi wa Cassie, Bongolan, Mia na wengineo.

Endapo Diddy atapatikana na hatia, anaweza kukabiliwa na kifungo cha muda mrefu jela au cha maisha jambo ambalo litakuwa na athari kubwa si tu kwa maisha yake binafsi bali pia kwa tasnia ya burudani ya Marekani.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags