2baba Afunga Ndoa Na African Queen Namba Mbili

2baba Afunga Ndoa Na African Queen Namba Mbili

Mkali wa Afrobeats kutoka Nigeria, Innocent Ujah Idibia maarufu kama 2Baba, ameripotiwa kufunga ndoa ya kimila na mpenzi wake mpya aitwaye Natasha Osawaru, sherehe ambayo ilifanyika Alhamis Julai, 25,2025.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa vyanzo vya karibu na familia hiyo, sherehe hiyo ya kitamaduni ilihudhuriwa na ndugu, jamaa wa karibu pamoja na wazazi wa 2Baba.

Licha ya taarifa za bibi harusi huyo mpya Natasha kutofahamika sana katika mitandao ya kijamii, kukubalika kwakwe na familia kumezua mijadala mitandaoni kutoka kwa mashabiki wakihoji hatua hiyo aliyoichukua 2Baba ikizingatiwa kuwa ni mume halali wa Annie Idibia, ambaye wamekuwa kwenye ndoa kwa muda mrefu.

Utakumbuka Februari 11, 2025 2Baba kupitia ukurasa wake wa Instagram alishare picha ya mwanadada huyo ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Edo, Natasha akimtambulisha kuwa ndio mwanamke ambaye atafunga naye ndoa kwa mara nyingine.

"Natasha ni mwanamke mchanga, mwelevu, na wa ajabu. Nampenda, anapendeza, na nataka kumuoa," amesema 2Face huku akisisitiza kuwa Mbunge huyo asihusishwe na talaka yake na badala yake lawama zote ziende kwake.

Msanii huyo aliyewahi kutamba na ngoma ya 'African Queen'. Mwishoni mwa Januari 2025 alitangaza kutengana na aliyekuwa mke wake baada ya kudumu naye kwa miaka 13.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags