Kwa sasa kusheherekea siku ya kuzaliwa ni jambo la kawaida duniani kote, lakini hapo zamani sherehe hiyo ilikuwa ikifanywa kwa ajili ya familia za Kifalme.
Kwa mujibu wa historia, utamaduni wa kusherehekea siku ya kuzaliwa ulianzia nchini Misri mwaka 3000 KK, ambapo Farao ndio anatajwa kuwa mtu wa kwanza kusherehekea siku hiyo tukio ambalo lilitajwa kuwa la kipekee nchini Misri.
Siku hiyo ilitambulika si tu kama siku ya kuzaliwa ya mfalme bali ilikuwa ni kuzaliwa upya kwa Farao ambapo katika mji huo kulifanyika sherehe kubwa iliyoambatana na Matambiko ya kidini, Sadaka kwa Miungu, Nyimbo, ngoma, kupokea zawadi na wakati mwingine Farao alitumia muda huo kutoa msamaha kwa wafungwa.
Aidha Wagiriki waliendeleza wazo hilo kwa kuanzisha sherehe za kuzaliwa kwa Miungu yao, hasa Artemis (Mungu wa kike wa uwindaji). Ambapo walipeleka keki zenye umbo la mwezi pamoja na mishumaa katika sanamu la Mungu huyo, ndipo wazo la keki ya kuzaliwa na mishumaa lilipoingia katika jamii.
Kwa upande wa Warumi wao walipanua wigo wa sherehe hizo ambapo walianza kusherehekea kwa wanaume huku wanawake wakikatazwa kusherehekea hadi ilipofikia karne ya 12. Ambapo mpaka kufikia sasa kila mtu anasherehekea siku hiyo.

Leave a Reply