Diddy aomba tena dhamana, aweka bondi nyumba yake

Diddy aomba tena dhamana, aweka bondi nyumba yake

Mkali wa hip-hop na mfanyabiashara kutoka Marekani, Sean “Diddy” Combs (55), ameiomba mahakama imwachie kwa dhamana ya dola milioni 50 pamoja na bondi ya nyumba yake iliyopo Miami huku akisubiri hukumu ya kesi yake.

Kwa mujibu wa wakili wa Diddy, Marc Agnifilo amedai mazingira ya Gereza la Metropolitan (MDC Brooklyn), ambapo yupo rapa huyo ni hatarishi kwa afya na usalama wake. Wakili huyo alihoji kwanini Diddy aendelee kuzuiliwa wakati watuhumiwa wengine wa awali walipatikana na hatia lakini waliachiwa huru kwa dhamana huku wakusubiri hukumu.

“Sean Combs hastahili kuwa jela kwa tabia hii, kwa kweli, huenda akawa mtu wa pekee kwa sasa aliyeko gerezani nchini Marekani kwa kuwa ‘John’ (mtu anayelipa watu kwa ajili ya huduma ya ngono), hasa kwa kuwa wanaume watu wazima waliofanya huduma za ngono kwa niaba yake na mpenzi wake,” alisema Agnifilo katika hoja alizowasilisha mahakamani Jumanne.

Hata hivyo, upande wa mashtaka umepinga ombi hilo ukisisitiza kuwa Diddy ni mtu mwenye ushawishi mkubwa na anaweza kutoroka kesi, hivyo hapaswi kupewa dhamana.

Ikumbukwe Diddy alipatikana na hatia mapema Julai kwa makosa mawili ya kusafirisha watu kwa ajili ya kushiriki katika vitendo vya ukahaba. Mahakama ilieleza kuwa aliwasafirirsha wapenzi wake wa zamani na watoa huduma wa kiumbe katika maeneo mbalimbali ya Marekani kwa ajili ya matukio ya kingono.

Aidha alifutiwa mashtaka matatu ikiwa ni pamoja na kula njama ya kufanya uhalifu (racketeering conspiracy), kulazimisha watu kwa ajili ya ngono mashtaka ambayo kama angepatikana na hatia kungekuwa na uwezekano wa kifungo cha maisha jela.



Mara baada ya kuondolewa mashitaka hayo Julai 2, 2025 wakili wake aliomba atolewe kwa dhamana, lakini Jaji Arun Subramanian alikataa, akisema ushahidi wa Diddy bado haupo wazi kwamba si hatari kwa mtu yeyote na jamii. Ambapo sasa wakili huyo amekuja tena na ofa nono ya dhamana ya dola milioni 50 pamoja na bondi ya nyumba ya Diddy iliyopo Miami.

Kwa sasa, Diddy ameingia katika orodha ya watu maarufu waliowahi kufungwa katika gereza la MDC Brooklyn. Gereza pekee la shirikisho jijini New York, ambapo mastaa wengine waliowahi kuwepo ni pamoja na mwimbaji R Kelly, Ghislaine Maxwell na mfanyabiashara wa sarafu ya kidijitali Sam Bankman-Fried nk. Diddy anatarajiwa kuhukumiwa Oktoba 3,2025.

Kuhusu Trump kutoa msamaha kwa Diddy

Naye Rais wa Marekani, Donald Trump, ameibua sintofahamu mpya kuhusu Diddy baada ya chanzo cha karibu na Ikulu kudai kuwa Rais huyo anafikiria kutoa msamaha kwa Diddy kufuatia na mashitaka yanayomkabili.

Inaelezwa kuwa Trump ameendelea kusisitiza kuwa msamaha wa Rais unaweza kutolewa lakini hakuna ndugu wala wakili aliyewasilisha ombi la kutaka msaada kwa Rais huyo.

Utakumbuka, Trump na Diddy walikuwa marafiki wa muda mrefu tangu miaka ya 1990 na walikuwa wakionekana mara kwa mara kwenye hafla za kifahari za Manhattan. Mwaka 2012, Trump alimtaja Diddy kama “rafiki mzuri.” Hata katika kipindi cha ‘The Apprentice’ msimu wa 12, alimwambia mwimbaji Aubrey O’Day kuwa “bosi wako wa zamani ni mtu mzuri, na nitamtetea kwa lolote”.

Urafiki wao ulipata doa baada ya Diddy kumuunga mkono Joe Biden mwaka 2020 katika uchaguzi huku akimkosoa Trump hadharani. Aidha licha ya tofauti hizo mwezi Mei Trump alionesha nia ya kutaka kumsaidia rapa huyo katika kesi yake.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags