Kupitia ukurasa wa Instagram wa Majizzo amashare orodha hiyo yenye nyimbo 20 ikiongizwa na wimbo wa Diamond ‘Komasava’ huku akiambatanisha na ujumbe usemao…
“Kwa kuwa mwaka unakaribia kumalizika, nilitaka kushiriki baadhi ya nyimbo ambazo nimekuwa nikisikiliza siku za hivi karibuni na isingekuwa orodha yangu ya nyimbo bila kuhusisha nyimbo za singeli. Natumaini utapata kitu kipya cha kusikiliza,” ameandika Majizzo

Ngoma nyingine ambazo zimeingia katika orodha hiyo ni pamoja na Hakuna Matata, Olodumare, Kautaka, Wivu, Pwita, Ova, Unanichekesha, Dah, Mapozi, Mungu Abless, Tera Ghata na nyinginezo.
Leave a Reply