Rapa kutokea nchini Marekani Nicki Minaj ameshtakiwa na aliekuwa meneja wake wa zamani Brandon Garret kwa kumshambulia na kumpiga hali iliyosababisha mfadhaiko wa kihisia kwa meneja huyo aliekuwa akisimamia ziara yake ya Pinky Friday 2 mwaka 2024.
Kulingana na hati za mahakama zilizodakwa na jarida la TMZ , Brandon alifungua kesi dhidi ya Nicki Minaji katika Mahakama ya Juu ya Los Angeles Ijumaa, Januari 3, 2025 akidai kwamba alipokuwa akifanya kazi kama meneja wa ziara ya Pink Friday 2, aligombana na Nick hali iliyopelekea kumtusi na kumpiga.
TMZ na Variety wana ripoti kuwa Kisa hicho kinachodaiwa, kilitokea kwenye ukumbi wa Little Caesars Arena huko Detroit Aprili 21, 2024 baada ya tamasha la Minaj kumalizika.
Mawakili wa Garrett wanadai katika malalamiko hayo meneja wa ziara hiyo alikuwa akielekea uwanjani wakati Mkuu wa usalama wa Minaj Larry Dathan alimtumia ujumbe mfupi akimtaka aongee na Minaj kwenye chumba chake cha kubadilishia nguo.
Garrett anaeleza kuwa wafanya kazi wengine wanane wa Minaj walikuwepo kwenye chumba hicho ndipo Minaj alianza kulalamika kuhusu baadhi ya wafanyakazi kutojua wanachotakiwa kufanya, na nani anaripoti kwa nani .katika malalamiko hayo menaja huyo anadai kwamba Minaj alionekana kuchukizwa sana na kumfokea kwa hasira akimwambia "Natamani meno yako yangekung'oka tu maisha yote, na hautakuwa mtu yeyote, nitahakikisha.
Minaj alimpiga kofi Garrett upande wa kulia wa uso wake na kusababisha kichwa chake kurudi nyuma huku kofia yake ikiruka kutoka kichwani," Wanasheria wa Garret waliimbia Variety.
Mawakili wa Garrett waliandika kwenye malalamiko hayo kwamba meneja huyo wa zamani wa Nick Minaji alijifungia bafuni kwa saa kadhaa baada ya tukio hilo na baadae akapokea ujumbe mfupi wa maandishi ukimwambia kwamba hatohitajika tena kwenye matamasha ya Ziara hiyo.
Hata hivyo meneja huyo wa zamani wa Nick Minaji aliwasilisha ripoti rasmi ya polisi huko Detroit, na mawakili wake sasa wanaomba malipo na adhabu itolewe kwa Rapa huyo kufuatia tukio hilo.
Kwa upande wa wakili wa Minaj, Judd Burstein aliiambia TMZ kwamba bado hajapokea malalamiko hayo, lakini alikanusha madai yaliyoripotiwa na chombo hicho.
"Kwa wakati huu hakuna malalamiko yoyote ambayo yametolewa kwa Minaj, kwahiyo hatujui madai maalum, " Wakili Judd allimbia TMZ.
Leave a Reply