Rais Samia Mgeni Rasmi Kwenye Ugawaji Tuzo Za Comedy

Rais Samia Mgeni Rasmi Kwenye Ugawaji Tuzo Za Comedy

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan ndio anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ugawaji wa tuzo za wachekeshaji ‘Tanzania Comedy Award’ zitakazotolea Jumamosi Februari 22, 2025 ‘Ware House Masaki’.

Taarifa hiyo imewekwa wazi usiku wa kuamkia leo Februari 27,2025 na Naibu Waziri wa habari tamaduni sanaa na michezo Hamis Mwinjuma ‘Mwanafa’ kwenye tamasha la ‘All Stars Comedy Festival’ lililofanyika Mlimani City ikiwa ni lapsha lapsha kuelekea siku ya ugawaji wa tuzo hizo.

Hata hivyo taarifa hiyo imepokelewa kwa furaha isiyo na kifani kutoka kwa wadau wa sanaa ya ucheshi lakini pia muanzilishi wa tuzo hizo Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ ameelezea furaha yake Rais Samia kuwa mgeni rasmi siku hiyo ya ugawaji wa tuzo.

“Kwanza nafuraha sana kwa sababu Serikali imeona kitu hiki ni kikubwa na kuamua kusapoti tasnia hii ya uchekeshaji na kuweza kulipa nguvu wazo tulionzisha.

Tulipo tuma maombi kwa Raisi wetu kama anaweza kuwa mgeni rasmi yeye mwenyewe ni shabiki wa komedi kwaiyo kiukweli mimi mwenyewe nimefurahi sana kama mnavyoona tumetuma maombi leo na leo leo Rais amekubali kuwa mgeni rasmi,” Amesema Ommy.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags