Rais wa kitaa na Messi wa bongo fleva wanajambo lao

Rais wa kitaa na Messi wa bongo fleva wanajambo lao

Mwanamuziki wa Hip-Hop Nay Wa Mitego na Rich Mvoko, wanatarajia kuachia ngoma yao hivi karibuni, itakayoenda kwa jina la #SioWewe,

Nay amedhihirisha ujio wa ngpma hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram, baada ya ku-post picha kiwa pamoja na Rich na kuisindikiza kwa ujumbe usomekao

"#RaisWaKitaa Na Mess Wa BongoFlavour #RichMavoko Now Ni Time Kuwarusha Kaeni Tayari Watu Wangu #SioWewe".

Ujio wa ngoma hiyo utakuwa unawarudisha mashabiki wa Rich kupata kile walichokuwa wanakikosa kwa mda mrefu kutoka kwa msanii huyo kwani tangu aachie ngoma ni miezi kumi na moja sasa imepita, huku kwa upande wa Nay aliachia wimbo uitwao 'Mamlaka' wiki tatu zilizopita.
.
.
.
#MwananachiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags