Msanii wa Hiphop nchini Tanzania, Rapcha ametangaza kwa mara ya kwanza kuachana na lebo ya muziki ya Bongo Record ambayo imekuwa ikimsimamia kwa muda mrefu.
Rapcha ameweka wazi kupitia mahojiano aliyoyafanya kwenye kipindi cha The Throne, Crown Media akisema kuwa mkataba wakufanya kazi na lebo hiyo umeisha.
"Sasahivi mimi ni msanii naejitegemea, sijavunja mkataba lakini naendelea tu kufanya kazi na Father majini kama family" amesema Rapcha.
Rapcha alisainiwa na lebo ya Bongo Record mwaka 2019 na amefanikiwa kutoa nyimbo nyingi ambazo zimefanya vizuri zikiwemo Lissa, Uwongo, Wait na nyingine nyingi lakini pia alifanikiwa kutoa Album 2 ambazo ni Wanangu 99 (2021) na To The Top Vol.2 (2023).
Leave a Reply