Rushwa Ya Ngono Ilivyomnyima Tuzo Yemi Alade

Rushwa Ya Ngono Ilivyomnyima Tuzo Yemi Alade

Mkali wa Afrobeat kutoka Nigeria, Yemi Alade amefunguka kuwa amekosa tuzo nyingi kutokana na kukataa kutoa rushwa ya ngono.

Wakati alipokuwa kwenye moja ya mahojiano yake Yemi amebainisha kwamba amekuwa akikataa maombi mengi ya rushwa ya ngono kutoka kwa watu mbalimbali ambao walimuahidi kushinda tuzo endapo angefanya nao kitendo hicho.

“Kulikuwa na wakati katika tasnia ambapo kila mtu alitaka kulala nami, na ilikuwa kama, ‘Yemi, usipofanya hivi, hutapata kile.’ Leo, wanaume ndio sababu sipati tuzo nchini Nigeria, kulala na wanaume kulionekana kama daraja nililopaswa kuvuka ili kupata fursa fulani, mikataba na hata tuzo.

Niliamua kutoshiriki mahusiano ya kingono kwa manufaa, na mara moja nafasi nyingi zilifungwa kwangu. Jiulize kwa nini Yemi Alade, ambaye ndiye msanii wa kike wa Nigeria mwenye watazamaji wengi zaidi na wanaofuatilia kwa wingi kwenye YouTube, hatambuliwi kwenye tuzo mwaka baada ya mwaka. Hata kwenye mijadala ya Twitter, hakuna anayemtaja Yemi Alade kama mmoja wa wasanii wa kike wakubwa zaidi nchini Nigeria,”amesema Yemi

Aidha aliongezea kwa kuandika “Wamenifungia kila kitu. Lakini nina furaha kwa sababu nina heshima yangu, nina maisha yangu, ninatengeneza pesa nzuri, na zaidi ya yote, nina mashabiki wanaonipenda sana,”

Hata hivyo, licha ya changamoto hizo, Yemi Alade ameendelea kung'ara katika tasnia ya muziki na kujizolea umaarufu mkubwa barani Afrika na duniani kote huku akinyakua tuzo mbalimbali ikiwemo Best Female katika tuzo za MTV Africa Music Awards, Best Female Western Africa (AFRIMMA Award), Female Artist of the Year(African Entertainment Awards USA (AEAUSA)).

Mbali na Yemi kuzungumza changamoto hiyo hadharani mastaa wengine ambao wamekumbwa na matatizo kama hayo ni pamoja na mwanamuziki Kesha ambaye alidai kwamba aliathiriwa na unyanyasaji wa kingono na mtayarishaji Dr. Luke, ambaye alimlazimisha kufanya vitendo vya ngono ili kupiga hatua katika tasnia.

Wengine ni pamoja na Lady Gaga, Nicki Minaj, Azealia Banks, Tinashe na wengineo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags