Kampuni ya simu Apple ambayo pia inatengeneza saa imezuiliwa kuuza ‘Apple Watch’ ambazo zimetengenezwa kwa mfumo unaopima kiasi cha Oxygen kwenye damu nchini Marekani.
Saa hizo aina ya Series 9 na Ultra 2 zimezuiliwa kuuzwa kutokana na madai ya kuiba mfumo huo kutoka kwa kampuni ya #Masimo, kufuatiwa na tuhuma hizo Apple imeshindwa kesi hiyo iliyosikilizwa siku ya jana Alhamis katika Mahakama ya Rufaa ya Marekani kutokana na kuiba haki miliki ya #Masimo.
Hivyo basi ili Apple iweze kuuza saa zake nchini Marekani inatakiwa kuzima mfumo huo kuanzia siku ya jana.

Leave a Reply