Sancho akalia kuti kavu Manchester United

Sancho akalia kuti kavu Manchester United

Inadaiwa kuwepo kwa taarifa za 'winga' wa ‘klabu’ ya #ManchesterUnited, #JadonSancho anaweza kuondoka Old Trafford  baada ya tovuti ya ESPN kuripoti baadhi ya wachezaji wenzake wamemkataa.

Mchezaji huyo huenda akatimkia Uturuki ambako dirisha la usajili  bado lipo wazi. Staa huyu hivi karibuni ameingia kwenye sintofahamu baada ya kudaiwa kutupiana maneno na 'kocha', Erik Ten Hag mara baada ya 'mechi' dhidi ya Arsenal.

Ingawa mkataba wa sasa wa Sancho unatarajiwa kumalizika mwaka 2026, ambapo  awali kulikuwa na 'ofa' kutoka Al-Ettifaq ya Saudi Arabia lakini dili hilo halikufanikuwa.Kwa sasa inaripotiwa kuna uwezekano Galatasaray na Fernebanhce zikamchukua kwa mkopo kwani uwezekano wa kucheza tena kwenye ‘klabu’ ya Man U ni mdogo kutokana na hali ilivyo sasa.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags