Selena Gomez, mwigizaji na mwanamuziki ambaye anaupiga mwingi katika tasnia ya burudani amefunguka kuwa itakuwa ni changamoto kwake kurudi kwenye muziki hii ni baada ya kufurahia mafanikio yake katika uigizaji.
Wakati alipokuwa kwenye tamasha la filamu la Kimataifa la ‘Santa Barbara’ ameeleza mustakabali wake katika muziki huku akidai kuwa anajivunia zaidi mafanikio yake katika filamu ya Emilia Pérez.
“Itakuwa vigumu sana kwangu kurudi kwenye muziki baada ya hili,” amesema Gomez
Emilia Pérez iliachiwa rasmi Agosti 2024 huku ikiongozwa na Tanya Hamilton, filamu hiyo ilifanikiwa kushinda tuzo nne za Golden Globe, vile vile iliteuliwa kuwania vipengele 13 katika Tuzo za Academy za 97.
Wimbo wa mwisho kuuachia katika mtandao wake wa kutazama na kusikiliza muziki wa YouTube ni ‘The Making of 'Love On'’ aliouachia miezi 10 iliyopita.

Leave a Reply