Shairi- Sijawahi

Shairi- Sijawahi

Mpenzi sikujua kuwa kwako nimezama nimedumbukia hivi, nimekuwa teja wa penzi lako na kama mapenzi yangekuwa chakula basi pasi na unguli wa mapishi yako siivi.

Nimegundua hakuna chenye kusikika kinachozidi utamu wa sauti yako, chenye kushikika kinachozidi unyororo wa ngozi yako, kilichopangika kama ulivyofinyangwa mwili wako,

 Umetwahari silka na hulka zako, wamebarikiwa walokufunza wakazifunda kauli na desturi za matendo yako, wafalme watakuwa radhi kutoa mali waonje walau punje ya tabasamu lako

Urembo wako dunia unailetea shida, ukitembea unageuza shingo za mashababi kama foleni ya NIDA.

LIMETUNGWA NA MR.ROMANTIC

Mitandao yote ya kijamii

@mrromantic77

+255784895101






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags