Sheikh Jassim hana habari tena na Man United

Sheikh Jassim hana habari tena na Man United

Mchakato wa uuzwaji wa ‘klabu’ ya Mancheste United umeingia doa baada ya mnunuzi kutoka Qatar aliyekuwa mstari wa mbele kwenye kinyang'anyiro cha kuichukua ‘klabu’ hiyo, Sheikh Jassim kujiondoa kwenye biashara hiyo  baada ya ofa yake mpya kutupiliwa mbali na wamiliki wa ‘klabu’ hiyo familia ya Glazers.

Inadaiwa kuwa Jassim aliongeza dau la kuinunua ‘klabu’ hiyo mpaka kufikia Pauni 5.5 bilioni sawa na Tsh 16.7 trilioni ,  wamiliki wa ‘klabu’ hiyo wamekataa ofa hiyo na kutaka  pauni  6 bilioni sawa na Tsh. 18.2 trilioni.

Aidha wahusika wa karibu wa Sheikh Jassim wamegoma kufichua undani wa habari hizo kwa madai ya vizuizi vya faragha lakini wamethibitisha kujiondoa kwenye mchakato wa kuinunua ‘klabu’ hiyo.

Sheikh Jassim ndiye alikuwa mnunuzi pekee aliyetaka kuinunua ‘klabu’ hiyo jumla huku Sir Jim Ratcliffe akitaka kununua sehemu ya hisa za Manchester United.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags