Moja ya show ambayo imekuwa ikifanya vizuri kila mwaka ni na Show ya Halftime ya Super Bowl ambayo imeonesha ukubwa wake katika ufuatilia kwenye mitandao ya kijamii huku show ya mwaka 2025 ikiivunja rekodi liyowahi kuwekwa miaka 30 iliyopita.
Show za mastaa hawa zimetazamwa zaidi Show ya Halftime ya Super
Namba moja inachukuliwa na mkali wa ‘Not Like Us’ Kendrick Lamar ambaye amepata watazamaji zaidi ya milioni 133.5 ndani ya siku mbili huku akimpiku marehemu mfalme wa pop Michael Jackson ambaye alikuwa akishikiria rekodi hiyo kwa miaka 30 ambapo alifanikiwa kuondoka na kijiji kwa kupata watazamani milioni 133.4.
Mbali na hao wawili kuliwakilisha vyema jukwa hilo lakini pia mwanamuziki Usher Raymond alifanikiwa kupata watazamaji 123.4, Rihanna ‘Riri’ akipata watazamaji milioni 121 huku katika historia ikionesha kuwa Riri hakuwa na tofauti na Katy Perry ambaye alipata watazamaji 121 mwaka 2015.
Aidha wasanii wengine ambao wamekiwasha zaidi ni Lady Gaga milioni 117.5, kundi la Cold Pay likiwa na watazamaji milioni 115.5, Bruno Mars milioni 115.3, huku listi hiyo ikimalizia wa msanii kutoka Uingereza Madonna ambaye alifanikiwa kupata watazamaji milioni 114.

Leave a Reply