Snoop Dogg: Kendrick Lamar wewe ni Mfalme

Snoop Dogg: Kendrick Lamar wewe ni Mfalme

Mwanamuziki wa Marekani Snoop Dogg amempa ‘rapa’ Kendrick Lamar maua yake kwa kumtaja msanii huyo kuwa ni mfalme wa Magharibi.

Kupitia video aliyopost Dogg kwenye instastory yake imemuonesha mwanamuziki huyo akimsifia Lamar kufuatia na show yake ya hivi karibuni huku akimpongeza kuwaunganisha wasanii wa magharibi ambao ni Dr Dre na The Weekend.

“Ni asubuhi na mapema Snoop Dogg naongea na nyinyi nikiwa Canada natuma pongezi nyingi kwa Kendrick Lamar wewe ni mfalme wa Magharibi umefanya vyema kuunganisha wasanii wa magharibi pamoja kwa ajili ya kuleta upendo na umoja”

Hii sio mara ya kwanza kwa Dogg kumwaga sifa kwa Lamar kwani wakati wa bifu la Lamar na Drake aliwapongeza wawili hao kurudisha muziki kwenye mstari.

Kendrick Lamar aliwapandisha jukwaani Dr Dre na The Weekend katika tamasha lake la ‘Pop Out’ lililofanyika Los Angeles, Marekani Juni 19 mwaka huu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags