Timu ya 76ers yapoteza tena mchezo wake

Timu ya 76ers yapoteza tena mchezo wake

Unaambiwa bwana hali imezidi kuwa mbaya kwa timu ya Philadelphia 76ers (Sixers) baada ya kupoteza mchezo wa pili wa nusu fainali kanda ya mashariki dhidi ya Miami Heats kwa kupoteza kwa alama 119-103 katika dimba la FTX Arena.

76ers wanaendelea kumkosa Joel Embiid ambaye ndiye mfungaji bora msimu huu, katika muendelezo wa mechi za nusu fainali baada ya kuumia kwenye mchezo wa robo fainali dhidi ya Toronto Raptors.

Nyota wa Miami, Jimmy Butler alikuwa mwiba mchungu kwa upande wa Philadelphia baada ya kufunga vikapu 22, asisti 15 na ribaundi 6 huku Bam Adebayo akifunga vikapu 23.

Kwa upande wa 76ers, jitihada za Tyrese Maxey aliyefunga vikapu 34 pamoja na James Harden aliandika alama 20 hazikuweza kuzaa matunda mbele ya mabingwa wa mwaka 2012 na 2013 waliokuwa na ngome imara ya ulinzi.

Mchezo wa tatu unatarajiwa kuchezwa siku ya jumamosi katika dimba la Wells Fargo Center, mchezo ambao utawalazimu 76ers kushinda ili kujihakikishia nafasi ya kurudi kwenye ushindani wa michezo saba ya nusu fainali.

 

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags