Travis Ashtakiwa kwa kuharibu ujauzito wa shabiki

Travis Ashtakiwa kwa kuharibu ujauzito wa shabiki

Msanii maarufu nchini Marekani Travis Scott anashatkiwa na mtu mwingine tena ajulikanaye kwa jina la Shanazia Williams aliyehudhuria tamasha lake kubwa duniani la mAstroworld.

Aliyemshtaki ni mwanamke ambaye anadai kuwa katika tamasha hilo kulitokea taharuki na watu kupata msukosuko akiwemo yeye aliyepata majeraha yaliyopelekea ujauzito wake kuharibika.

Mwanamke huyo amedai kuwa alihudhuria tamasha la Travis mwaka jana na ghafla alikanyagwa wakati wa taharuki kubwa ilipotokea na kupatamajeraha yaliyopelekea ujauzito wake kuharibika.

Katika nyaraka zilizodakwa na TMZ zilieleza kuwa mwanamke huyo na mumewe wanadai kuwa hakukuwa na usalama wala kuwekwa mfumo mzuri wa kusimamia tamasha hilo ambalo lilikuwa sababu ya Williams kujeruhiwa pamoja na kifo cha mtoto wake ambaye hajazaliwa.

Mbali na kuharibika kwa ujauzito wa mwanamke huyo alidai kuwa majeraha mengine aliyapata begani, mgongoni, kifuani, mguuni, tumboni na sehemu zingine za mwili wake.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags