Tyla awapiga chini Burna Boy, Chris Brown, Usher

Tyla awapiga chini Burna Boy, Chris Brown, Usher

Mwanamuziki wa Afrika Kusini Tyla amewapiga chini kwa mara nyingine wasanii wenzake katika Tuzo za MTV VMAs 2024 kipengele cha Best Afrobeats zilizotolewa usiku wa kuamkia leo Septemba 12.


Tyla kupitia wimbo wake ‘Water’ ameibuka kinara kwa mara nyingine huku akiwapiku mastaa aliokuwa akichuana nao kama Ayra Starr (Last Heartbreak Song) , Burna Boy (City Boys) Chris Brown (Sensational), Tems (Love Me JeJe) , na Usher (Ruin).


Hii itakuwa tuzo ya pili kubwa kuipata kupitia wimbo huo kwani mwezi Februari ‘Water’ ilichukua tuzo ya Grammy katika kipengele cha ‘Best African Music Perfomance’.


Aidha katika tuzo hizo kwenye kipengele cha ‘Best Afrobeat’ waliokuwa wanawania tuzo ni pamoja na Usher, Davido, Burna Boy, Ayra Starr, Lajoy, Giveon, Pheelz na Tems.

Mbali na hayo wakati wa kupokea tuzo hiyo Tyla amezungumzia kuhusu wasanii wa Afrika kuwekwa kwenye kundi moja na kutaka jambo hilo likomeshwe kwani muziki wa Afrika unaweza kuwa muziki wa Pop pia.


Utakumbuka kuwa wimbo wa ‘Water’ ulitoka rasmi Oktoba 2023 huku video ya wimbo huo ikiwa na zaidi ya watazamaji milioni 230 katika mtandao wa YouTube.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags