Tyla Msanii Bora Wa Dunia, Tuzo Za Iheart

Tyla Msanii Bora Wa Dunia, Tuzo Za Iheart

Usiku wa kuamkia leo zimegawiwa Tuzo za Iheart Radio Music Award, zilizofanyika katika ukumbi wa Dolby Theatre, Los Angeles Marekani zikiongozwa na mshereheshaji LL Cool J. Huku mastaa mbalimbali wa muziki wakihudhuria akiwemo Nelly na mpenzi wake Ashanti.

Katika tuzo hizo ambazo huangazia nyimbo zilizochezwa zaidi katika jukwaa hilo kwa mwaka mzima. Tylor Swift na Morgan Wallen ndiyo walikuwa vinara kwa wasanii walioteuliwa kuwania vipengele vingi.

Wakali hao waliwania vipengele kumi kwa kila mmoja wakifuatiwa na Kendrick Lamar, Post Malone na Sabrina Carpenter ambao wote walikuwa wakiwania vipengele tisa kwa kila mmoja wao.

Wasanii waliotumbuiza katika tuzo hizo ni pamoja na Billie Eilish, Bad Bunny, GloRilla, Gracie Abrams, Kenny Chesney, Muni Long na Nelly. Katika usiku huo wasanii wa kike wa tatu walitunukiwa tuzo za heshima.

Wasanii hao ni Lady Gaga alipokea tuzo ya Mvumbuzi bora 2025, Mariah Carey alipokea Tuzo ya iHeartRadio Icon Award 2025, na Taylor Swift ilipewa tuzo ya Tour bora ya Karne (licha ya kuwa ndio kwanza tupo kwenye robo ya karne hii ya 21).

Lakini pia, rapa na mwimbaji kutokea Marekani Nelly alipokea Tuzo ya iHeartRadio Landmark Award, ikiwa ni kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 25 ya albamu yake ya kwanza inayoenda kama 'Country Grammar' iliyoachiwa 2000.

Tuzo hizo pia zimeangazia wasanii wa Afrika kwa kuwapa nafasi ya kushiriki kwenye vipengele mbalimbali ikiwemo kipengele kikubwa zaidi cha Msanii Bora Wa Dunia ambapo kwa mwaka 2025 ameshinda Tyla kutokea Afrika ya Kusini akiwashinda wasanii wengine kama Burna Boy (Nigeria)Central Cee (UK), Tems (Nigeria), YG Marley.

Tyla ndio msanii pekee kutokea Afrika aliyekuwa akiwania vingele vingi zaidi, alikuwa akiwania vipengele vitatu katika tuzo hizo ambavyo ni Msanii Bora wa Dunia wa Mwaka, Wimbo wa R&B wa Mwaka na Wimbo Bora wa kuchezeka wa Mwaka. wasanii wengine waliyo wakilisha Afrika kwenye tuzo hizo ni pamoja na Burna Boy, Tems, Davido, na Lojay

Hata hivyo, washindi wa tuzo hizo kutoka vipengele mbalimbali ni pamoja na Taylor Swift aliyeshinda Msanii Bora wa Mwaka akiwashinda wasanii wengine ambao ni Billie Eilish, Doja Cat, Jelly Roll, Kendrick Lamar, Post Malone, Sabrina Carpenter, na SZA.

Tuzo ya Wimbo Bora wa Mwaka ilienda kwa 'Benson Boone' kupitia wimbo wake wa 'Beautiful Things', ukizishinda nyimbo zingine kama 'A Bar Song (Tipsy)' ya Shaboozey, 'Agora Hills' ya Doja Cat, 'Espresso' ya Sabrina Carpenter, 'Greedy' ya Tate McRae, 'I Had Some Help' ya Post Malone featuring Morgan Wallen, 'Lose Control' ya Teddy Swims, 'Lovin on Me' ya Jack Harlow, 'Not Like Us' ya Kendrick Lamar, 'Too Sweet' ya Hozie.

Wimbo Bora wa Kushirikiana ulishinda wimbo wa “Die With a Smile” wa kwao Lady Gaga na Bruno Mars huku ukizipiga chini nyimbo kama “Fortnight” ya Taylor Swift featuring Post Malone, “I Had Some Help” wakwake Post Malone featuring Morgan Wallen, “Like That”wakwao Future, Metro Boomin na Kendrick Lamar, “Miles on It” wa kwao Kane Brown na Marshmello.

Lakini pia, Mtayarishaji Bora wa Mwaka katika tuzo hiyo aliibeba Julian Bunetta akiwashinda Jack Antonoff, Evan Blair, Mustard, Dan Nigro. Na wimbo Bora wa Hip hop tuzo hiyo ilichukuliwa na wimbo wa “Not Like Us” wa kwake Kendrick Lamar na kwenye kipengele hicho ilikuwa ikichuana na nyimbo kama “Like That' yakwao Future, Metro Boomin na Kendrick Lamar, “Lovin on Me” ya kwake Jack Harlow, “Rich Baby Daddy” yake Drake featuring Sexyy Red na SZA lakini pia wimbo wa “TGIF” wa kwake GloRill.

Tuzo ya msanii Bora wa Hiphop ilienda kwa mwanadada GloRila ambaye kupitia kipengele hicho kizito alikuwa akishindana na vidume vitupu ambao ni Drake, Future, Kendrick Lamar na Travis Scott.

Tuzo ya Msanii Bora wa R&B ilinyakuliwa na SZA akiwashinda wenzake ambao ni Chris Brown, Muni Long, Usher, Victoria Monét. Hatahivyo Wimbo Bora Wa R&B umechukua “Made for Me” wa kwake Muni Long, “ICU” wa kwake Coco Jones, “Sensational” wake Chris Brown, Davido na Lojay, “Water” wa Tyla, “WY@” wa kwake Brent Faiyaz






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags