Mwanamuziki na mfanyabiashara Selena Gomez ameshindwa kuvumilia na kuamua kumwaga machozi kuhusiana na uamuzi wa Rais wa Marekani Donald Trump kuwatimuwa wahamiaji.
Kupitia ukurasa wa Instagram wa msanii huyo amechapisha video ikimuonesha akimwaga machozi na kulaani tukio hilo ambalo limeibua hofu kwa familia kutengana.
“Watu wangu wote wanashambuliwa, watoto, sielewi samahani sana, natamani nifanye kitu lakini siwezi. Sijui la kufanya. Nitajaribu kila kitu, naahidi,” Gomez alisema hilo kwenye video ambayo ameifuta kutokana na maoni mabaya ya watu.
Utakumbuka siku chache baada ya Rais huyo kuapishwa alitoa amri ya kuwarudisha wahamiaji kwenye nchi zao huku jeshi la Marekani likiwasafirisha zaidi ya raia 80 wiki iliyoisha.
Mwanamuziki huyo naye alihamia Marekani akitokea Mexico mwaka 1970 bila ya kuwa na hati maalumu za uhamiaji, huku toka wakati huo amekuwa akitetea haki za wahamiaji.
Leave a Reply