Uchumi 2023 utakuwa bora Zaidi, Ulaya

Uchumi 2023 utakuwa bora Zaidi, Ulaya

Mkuu wa Benki Kuu nchini Ulaya, Christine Lagarde amesema, uchumi wa kanda ya Ulaya utakuwa bora zaidi mwaka huu kinyume na ilivyohofiwa awali.

Lagarde ameyasema haya huko Davos Uswisi kunakoendelea kongamano la uchumi duniani ambapo kuna matumaini ya nchi kukwepa mgororo wa uchumi.

Aidha Mkuu huyo amesema nia ya Benki Kuu ya Ulaya ni kuurudisha uchumi hadi 2% na kuchukua hatua zote zinazostahili ili kufikia lengo, licha ya changamoto ya mfumuko wa bei unaoshuhudiwa hivi sasa.

Kulingana na makadirio yake, Benki Kuu ya Ulaya inatarajia kuwepo na ukuaji wa uchumi katika kanda hiyo kwa asilimia 0.5. Matumaini hayo ingawa yenye tahadhari yameanza wakati ambapo bei za juu za nishati zilizopanda mwaka jana kutokana na vita nchini Ukraine, zikianza kushuka.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags