Msanii wa Bongo Fleva, Jay Melody ametangaza album yake ya pili kukamilika ikiwa ni mwaka mmoja umepita tangu alipoachia album ya kwanza inayofahamika kama Therapy iliyotoka April 26, 2024.
Kupitia InstaStory, Jay Melody amewafahamisha mashabiki wake kuwa albamu hiyo mpya ipo tayari, huku akiahidi kuanza kuziporomosha nyimbo muda wowote kuanzia sasa
Ingawa msanii huyo bado hajataja jina la albamu hiyo mpya wala orodha kamili ya nyimbo 'Track List' lakini ameonesha matarajio makubwa ikizingatiwa mafanikio ya Therapy ambayo ilijumuisha nyimbo zilizotamba kwenye chati mbalimbali.
Album yake ya Therapy ilisheheni nyimbo 14 ambazo ni pamoja na Bado, Forever, Nahodha, Wa Peke Yangu, Usiniache, 18, Unanimaliza na nyingine nyingi.
Uwezo wake wa kuandaa album ndani ya mwaka mmoja baada ya album yake ya kwanza kutoka inaonesha ukomavu na ukuaji wake katika tasnia anayofanya.

Leave a Reply