Ed Sheeran Alivyopoteza Uwezo Wa Kuona Kisa Snoop

Ed Sheeran Alivyopoteza Uwezo Wa Kuona Kisa Snoop

Msanii maarufu kutoka Uingereza, Ed Sheeran amefichua kuwa aliwahi kupoteza uwezo wa kuona kwa muda baada ya kuvuta bangi akiwa na rapa nguli wa Marekani, Snoop Dogg.

Sheeran, aliyejizolea umaarufu zaidi kwa kibao chake ‘Shape of You’, ameeleza tukio hilo kupitia ukurasa wake wa TikTok hivi karibuni, ambapo alichapisha video akiwa na Snoop Dogg, ambaye alionekana akifunga kile kilichodhaniwa kuwa ni bangi.

Katika video hiyo, Sheeran ameandika, “Mara ya mwisho nilipovuta na Snoop nilipoteza uwezo wa kuona.”

Ingawa haikufahamika wazi ni lini tukio hilo lilitokea, kauli hiyo imeibua mjadala mitandaoni kuhusu athari za matumizi ya bangi, hasa kwa watu wasiokuwa na mazoea nayo.

Hii si mara ya kwanza kwa Snoop Dogg kuhusishwa na bangi. Mwaka jana, alizua taharuki baada ya kutangaza kuwa ameacha kuvuta, lakini baadaye alifafanua kuwa alikuwa akizungumzia kuachana na jiko la mkaa katika tangazo la biashara.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags