Ukaribu wa Drake na mtoto wake wazidi kushamiri

Ukaribu wa Drake na mtoto wake wazidi kushamiri


Rapa kutoka Canada, Drake ameonekana kuwa na ukaribu zaidi na mtoto wake wa kiume aitwaye Adonis licha ya kutengana na mama wa mtoto huyo Sophie Brussaux.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Drake ameshare barua aliyotumiwa na mtoto wake huyo akimshukuru baba yake kwa kumpa maisha na familia nzuri.

“Asante kwa kunipa maisha mazuri na familia yenye upendo. Nakupenda baba” aliandika Adonis mtoto wa drake




Sio mara ya kwanza kwa Drake kuonesha ukaribu wake na mwanae kwani amekuwa akishea matukio mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii wakiwa pamoja, mwezi October 2024 alionesha baadhi ya picha matukio ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa ya Adonis aliosherehekea kutimiza umri wa miaka 7.

Adonis amekuwa msaada kwenye ubunifu wa muziki wa baba yake, akiwa na miaka 5 alitokea kwenye video ya drake iitwayo “8 Am in charlotte” lakini pia ndie alibuni kava ya albam ya “ for all dogs”.

Vilevile alipokuwa akisheherekea kutimiza umri wa miaka 6 Drake alisimamia wimbo wa mwanae huyo mpaka kutoka unaofahamika kama “My Man” aliomshirikisha LP.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags