Muigizaji na producer kutoka nchini #Marekani #VinDiesel anakabiliwa na kesi ya udhalilishaji wa kingono kwa aliyekuwa msaidizi wake aitwaye #Jonasson.
Mkali huyo wa 'Fast & Furious' naye ameingia katika orodha ya ma-star wanaokabiliwa na kesi za unyanyasaji wa kingono baada ya #Jonasson kudai kuwa #Diesel alimlazimisha kufanya naye mapenzi bila makubaliano.
Kufuatiwa na nyaraka za kisheria zilizowasilishwa mahakamani zimeeleza tukio hilo lilitokea mwaka 2010 wakati wa uandaji wa filamu ya ‘Fast 5’ ambapo #Jonasson aliajiriwa na kampuni ya ‘One Race’ kama msaidizi wa #Diesel huku nyaraka hizo zikieleza kuwa tukio hilo lilitokea katika chumba cha muigizaji huyo kwenye hoteli ya ‘St Regis’ jijini #Atlanta.
Aidha mwanadada huyo amedai kuwa alikaa kimya muda wote kwa kuogopa nguvu na ushawishi mkubwa alionao muigizaji huyo.

Leave a Reply