Vita ya muziki Bongo, Harmonize akaa kando

Vita ya muziki Bongo, Harmonize akaa kando

Siku za hivi karibuni wasanii wengi #Bongo wamechachuka kwa kutoa nyimbo mpya na kushindana kushikilia trending kwenye mtandao wa #Youtube, ambapo jana msanii #AllyKiba ameachia kichupa chake kipya cha Amapiano huku mkali #Diamond akiendelea kukiwasha kwa kuendeleza mvua ya mawe aliyoisema.

Kwa upande wamashabiki wamecharuka na kuuliza kwanini msanii #Harmonize yuko kimya sana wakati wasanii wengine wakiachia kazi zao kila kukicha.

Ukipita mjini #YouTube, kazi ya mwisho kuachiwa na #KondeBoy ni wiki nne zilizopita, wakati ukipita kwa #Simba ni siku mbili tangu kuachia kichupa cha wimbo wake unaoenda kwa jina la #Shu huku #KingKiba ngoma yake ya #Sumu ndiyo kwanza yamotoo hata masaa 24 haijafikisha.

Je unadhani ukimya wa Harmonize unaashiria nini?






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags