Vitu vya kuwa navyo makini unapokuwa chuo

Vitu vya kuwa navyo makini unapokuwa chuo

Ooooooh! Wanangu sana kama kawaida yetu, najua ni week kadhaa zimepita tangu muanze maisha mapya ya chuoni na wengine ndo mnaendelea kulisongesha gurudumu la elimu mpaka joho livaliwee, aloooh! Sasa leo tumekuja na jambo ambalo utaweza kujifunza hususani kwa wale wanaoingia chuo kwa mara yao ya kwanza.

Hongera kwa kufika chuo tena, sehemu yenye uhuru na maamuzi unayoyafanya mwenyewe hata kama familia yako ipo ila kwa sasa wewe ndo utataka lipi liwe na lipi lisiwe, Hakuna kitu kizuri kama hicho kwenye maisha, kuwa huru katika yote chuoni.

Leo ningependa kukuambia vitu 5 vya kuwa navyo makini unapokuwa chuo, vya kuviangalia kwa jicho la tofauti maana vina umuhimu kwenye maisha yako ya chuo na ya baadae kwa ujumla.

  • Marafiki utakaouchagua

Kuna msemo unasema “nionyeshe marafiki zako watano, nami nitakuambia wewe ni mtu wa aina gani,” lakini pia watu husema, marafiki utakaowatengeneza chuo unaweza kudumu nao mpaka milele,” inawezekana ni kweli au sio kweli lakini nakubaliana sana na misemo hiyo.

Chuoni ni sehemu ambako nimetengeneza urafiki, tena wa kweli. Kuwa makini na kuchagua marafiki wako hasa sasa. Watu utakaowapata chuo wanaweza kukusababisha ufanikiwe au usifanikiwe kwenye maisha kwahiyo kuwa makini na chaguzi yako. Ni kheri uonekane ni mmbaguzi ila unafanya jambo sahihi kwa ajili ya maisha yako.

 

  • Kuzingatia masomo yako

Kuna watu wanasema GPA haina umuhimu. Inawezekana ni kweli au si kweli, lakini kumbuka sababu kuu iliyokupeleka chuo ni kusoma, kwahivyo kuwa makini na masomo yako, ni heri kuona GPA haina umuhimu ukiwa nayo nzuri, kuliko usipokuwa nayo nzuri. Mimi nimepata cheti changu kuna muda nikikiangalia natamani niongeze point 1 tu ili nibadilishe class kabisa. Pambana na masomo utoke na GPA nzuri.

  • Kuchunga matumizi ya hela

Hivi karibuni nimepiga mahesabu ya hela nilizokuwa nazipata nikiwa chuoni na nikagundua kuwa kama ningekuwa mtumiaji mzuri ningekuwa hata bilionea (au hata milionea basi au hata nina hela kidogo), lakini sikuwa na huo ufahamu au hata sikupewa ushauri toka naanza chuo. Lakini sitaki wewe upitie njia hiyo hiyo, maana unaweza ukakosa hata nauli ya kusambazia hiyo barua ya kuombea kazi ukimaliza chuo.

Unaweza ukawa na matumizi mazuri ya hela ukiwa chuoni kwa:

  • Kuwa na budget ya matumizi ya hela zako.
  • Kufungua biashara ambazo zitakuingizia kipato (salon na biashara ya chakula ni biashara maarufu sana maeneo ya chuo hili nilishalielezea kwenye mada iliopita kama bado hujasoma basi nenda kaisome ili upate ufahamu zaidi)
  • Kukaa na marafiki zako sehemu moja ili kusave hela.
  • Kufungua savings account au fixed account kwaajili ya pesa zako. Saving account usiiiguse kabisa, utahifadhi tu hela na fixed itakusaidia kuongeza hela baada ya kuiacha kwa muda.
  • Kuweka bill (mimi sikuweka bill, ila walioweka bill wanasema iliwapunguzia gharama za maisha)
  • Kujali afya yako

Kuwa makini na afya yako labda ningeweka kama kitu cha kwanza kwasababu chuoni unapitia/utapitia vingi sana vitakavyokuletea msongo wa mawazo kwenye maisha yako hapo chuo. Kumbuka unadili na masomo lakini wakati huohuo kuna familia inakuzunguka, mahusiano, drama za marafiki lakini siku nyingine unakuwa tu umechoka, kuwa makini na afya yako kwasababu hakuna umuhimu wa wewe kuugua au kupata matatizo eti kisa unasoma sana  na hata hivyo ukiugua hauwezi hata kusoma. Hivyo kuwa makini na afya yako, kimwili, kihisia, kiroho, kijamii na kisaikolojia.

Unaweza kufanya mambo yafuatayo katika kukusaidia kuwa makini na afya yako:

  • Kufanya mazoezi.
  • Kunywa maji, kula vizuri, kupumzika muda wa kutosha (masaa nane)
  • Kutoka nje ya mazingira ya chuo, kutembelea vivutio, beach nk.
  • Kukutana na marafiki, hakikisha una mtu hata mmoja unayemuamini kushirikiana naye unapopitia matatizo.

 

  • Image yako

Kuwa makini sana na image yako unapokuwa chuoni. Siri moja katika maisha ni kwamba hakuna watu wapya (zaidi ya waliozaliwa), hao uliotoka nao primary wengine mnakutana chuo au mtakutana ofisini au uliokutana nao chuo watakutana ofisini na watu uliosoma nao primary, kwahiyo kuwa makini na image yako unayoiweka mbele za watu.

Hapa simaanishi uigize maisha ya watu ambayo siyo yako na simaanishi ubadilishe maisha yako ili uonekane perfect, namaanisha maisha yenye taarifa mbaya, au image mbaya ambayo watu wataipata kuhusu wewe.

Hizo ndio tips chache tu kwako mwanachuo. Ukizingatia haya, hakika utatoboa katika Maisha yako ya chuoni na hata nje ya hapo.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags