Wanafunzi kutoka Sudan wawa gumzo mitandaoni

Wanafunzi kutoka Sudan wawa gumzo mitandaoni

Hahahah! Kama kawaida bongo hatunaga jambo dogo, baada ya kutangazwa taarifa masaa machache yaliyopita kuhusiana na wanafunzi kutoka nchini Sudani kuhamishiwa Tanzania.

Gumzo hilo limetokea kupitia mitandao ya kijamii baada ya wanafunzi hao 150 wa udaktari kutoka Chuo Kikuu cha Tiba Sayansi na Teknolojia (UMST) kuwa na muonekano mzuri au waswahili wanasema watoto wazuri.


Huku baadhi ya mastaa wa bongo kuweka utani katika picha za warembo hao, akiwemo Diamond katika komenti akiandika kuwa “leo nimeamka najiskia kama kahoma homa, nafikiri nahitaji vipimo hospitali ya Taifa” ameandika Diamond, akionesha kuvutiwa nao.

Kama kawaida utani huu unaendelea kupitia mitandao ya kijamii, je umeshakutana na posti ya wadada hao kupitia status au mitandao ya kijamii, dondosha komenti yako hapo chini utujuze kwa upande wako umeona nini kupitia wanafunzi hao.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags