Apple, SpaceX, na T-Mobile wameungana katika ushirikiano wa kimkakati ili kuboresha mawasiliano kwa watumiaji wa iPhone.
Kupitia ushirikiano huu, iPhone zenye toleo jipya la programu (iOS 18.3) sasa zinaweza kuunganishwa na mtandao wa ‘setilaiti’ wa Starlink wa SpaceX, kupitia huduma ya T-Mobile.
Ambapo watumiaji hao wataweza kutuma ujumbe wa maandishi kupitia setilaiti za Starlink hata wakiwa katika maeneo ambayo hayana mtandao wa kawaida wa simu.
Aidha baada ya kufanikiwa hilo waunganishaji wa Setilaiti hiyo wanaeleza kuwa kwa sasa wanawekeza zaidi nguvu zao ili watumiaji wa program hiyo waweze kupiga simu na kutumia data hata sehemu zisizo na mtandao siku zijazo.
Kwa sasa huduma hii inapatikana wa watumiaji wa Apple wa Marekani huku kukiwa na matarajio ya kupanua huduma hiyo iweze kusambaa kimataifa.

Leave a Reply