Will Smith Aendelea Kumgannda Jada

Will Smith Aendelea Kumgannda Jada

Kumekuwa na minong’ono kuwa mwigizaji na mwanamuziki Will Smith bado anamganda aliyekuwa mkewe Jada Pinkett Smith licha ya wawili hao kutangaza kutengena mwaka 2023.

Kwa mujibu wa chanzo cha karibu cha Smith kiliiambi tovuti ya People kuwa licha ya kutangaza kutengena kwao lakini maisha yao yanaendelea kama zamani.

“Liite unavyotaka. Wanaishi maisha yao tofauti lakini bado hawajakata uhusiano kabisa, bado wako pamoja, lakini kuhusu kuishi pamoja, wamekuwa na makazi tofauti kwa miaka mingi,” kimesema chanzo hicho

Wawili hao ambao walifunga ndoa tangu mwaka 1997, utengeno wao ulipewa msisitizo zaidi na Jada kupitia kitabu chake cha ‘Worthy’ (2023) akifunguka kuwa moja ya sababu inayowafanya wawe pamoja ni upendo wa kina.

“Bado tunajaribu kuelewa hali hii, tumekuwa tukifanya kazi kubwa sana pamoja. Tuna upendo wa kina kwa kila mmoja na tunajitahidi kutambua jinsi itakavyokuwa kwetu, Nitakuwa upande wake lakini pia nitampa nafasi ya kusuluhisha hili mwenyewe,” alisema Jada kupitia kitabu chake

Aidha kwa mujibu wa chanzo hicho kinaeleza kuwa Will ambaye ametangaza kurudi kufanya muziki yupo bize na majukumu yake ya kila siku ya kutengeneza filamu huku kukiwa na madai kuwa mke wake Jada anahangaika na michepuko.

Utakumbuka kuwa Oktoba 2023 mke wa Will Smith, Jada Smith alitangaza kutengana kwa siri na mumewe huyo miaka nane iliyopita huku akidai kuwa wawili hao hawana mpango wa kupeana talaka.

Will na Jada wamejaaliwa kupata watoto wawili ambao ni Jaden, mwenye umri wa miaka 26, na Willow, mwenye umri wa miaka 24, familia hiyo walionekana pamoja mara ya mwisho kwenye uzinduzi wa filamu ya Will ‘Bad Boys: Ride or Die’ iliyoachiwa Mei 2024.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags