Tunaweza kusema kila ifikapo Desemba, shamrashamra huwa nyingi kutokana na sikukuu ya Krismasi ambayo hufanyika duniani kote kila ifikapo tarehe 25 mwezi huo.
Upekee wa mwezi huo hutokana na shangwe ya baadhi ya watu ikisindikizwa na nyimbo maalum za mwezi huo. Kati ya nyimbo ambazo husikika kila kona kila ifikapo Desemba ni ‘Jingle Bells’ wimbo uliojizolea maarufu duniani.
Licha ya kuwa wimbo huo umekuwa ukitumika kama sehemu muhimu za sherehe hiyo, lakini historia yake inaeleza kuwa awali haukuandikwa kwa ajili ya sikukuu hiyo.
‘Jingle Bells’ ulitungwa mwaka 1857 na James Lord mwandishi wa nyimbo na mchoraji kutoka Marekani, akautumbuizwa kwa mara ya kwanza Septemba 15, 1857. aliuandika wimbo huu akiwa mji wa Medford, Massachusetts, na ulikusudiwa kuwa wimbo wa sherehe ya shindano la farasi kwa ajili ya kutumbuiza katika sherehe ya ‘Thanksgiving’ na sio kwa ajili ya Krismasi.
Wakati huo wimbo huo ‘One Horse Open Sleigh,’ kadri miaka ilivyozidi kwenda, uligunduliwa kuwa unaendana na maadhimisho ya Krismasi. ‘Jingle Bells’ ilijulikana kama wimbo wa Krismasi kwa sababu ya muktadha wa mapambo ya Krismasi, kama vile kengele, theluji, na sherehe za msimu wa baridi.
Umaarufu wa ‘Jingle Bells’
‘Jingle Bells’ ilianza kupata umaarufu kadri miaka ilivyozidi kwenda. Watu wengi walitokea kuupenda melodi zake kuwa nyepesi ikafanya kuwa rahisi watu kutoka sehemu mbalimbali duniani kuuimba na kuitumia katika sherehe za Krismasi.
Mwaka 1906, ‘Jingle Bells’ ulikuwa wimbo wa kwanza kuchezwa kwenye redio. Uchezaji huu wa kwanza kwenye redio ulisaidia kusambaa zaidi na kuongeza umaarufu wake.
Leo hii, ‘Jingle Bells’ inajulikana kama wimbo wa Krismasi na inachezwa katika redio, maduka, na sherehe nyingi za msimu wa Krismasi.
Matumizi ya wimbo katika sherehe za Krismasi
Maudhui ya kengele, yanayozungumziwa katika wimbo huo na mapambo ya Krismasi, ni jambo ambalo linavutia wengi. Vilevile, rithm ya wimbo huu huwapatia wasikilizaji wake furaha, huku ikimwongoza mtu kujumuika na wengine katika kusherehekea kipindi cha Krismasi.
Hata hivyo, licha ya kuwa wimbo huu mara nyingi umehusishwa na Krismasi, ‘Jingle Bells"’ pia unaweza kuimbwa wakati mwingine wowote, kama vile katika matukio ya furaha na sherehe nyingine, kwa kuwa ni wimbo unaoamsha hisia za furaha na umoja.
Leave a Reply