Wolper akana kujinunulia pete

Wolper akana kujinunulia pete

Msanii wa Filamu nchini Jackiline Wolper amefunguka na kuweka wazi kuwa pete ya uchumba aliyovishwa na mchumba wake Richmitindo ajajinunulia.

Wolper amesema mchumba wake Richmitindo aka baba P sio mario anaweza kununua pete na pia yeye anasifa ya kupendwa na si kujitongozesha.

Msanii huyo amefunguka hayo kupitia katika ukurasa wake wa Instagram baada ya watu kuongea maneno mengi huko mitandaoni ambayo yamemgusa na hivyo kuwajibu.

“Kwanza nijinunulie pete kwani mimi ndo nilianza kumtongoza jamani, ebu achene kukariri maisha wala msijali na nyie mtapendwa kama mimi na mtavishwa pete kama mimi ni suala la muda tu,” ameandila

Mwanadada huyo amesema amevishwa pete na mwanaume aliyemzalisha kitu ambacho si rahisi kwa maisha ya ujana aliyonao kwa maana wengi wamekuwa wakizalishwa na kutelekezwa lakini kwake kuna mwanga tayari juu ya mwanaume huyo.

“Nimevishwa pete katika muda sahii kwetu pengine pete nilizowahi kuvishwa awali muda haukuwa sahihi ndio maana hatukuweza kufikia malengo sio kwa ubaya.

“Sikutegemea kabisa kutokana na story zetu ndani….mara nyingi tulikuwa tunaongelea kuhusu biashara zetu kila siku tufanye nini ili tuweze kuongeza pesa zaidi, tufanye nini ili mtoto wetu P akute maisha mazuri zaidi,” ameandika Wolper

Wolper amewaomba mashabiki zake wazidi kumuombea isiishie kwenye pete tu bali ifike hatua ya ndoa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags