Mzalishaji muziki maarufu nchini S2kizzy ‘Zombie’ ameendelea kujimwagia maua yake huku akidai hakuna producer mwingine kutoka Bongo anayeweza kumfikia.
Zombie ameyasema hayo wakati alipokuwa kwenye mahojiano na waandishi wa habari usiku wa kuamkia leo Machi 21, 2025 kwenye shughuli ya ufuturishaji iliyoandaliwa na Diamond.
“Ushindani upo lakini sijaona Producer ambaye anafanya vitu ambavyo nafanya mimi. Kila mtu ana sound yake na nafasi yake, but kwangu mimi am the best toka tasnia ya East Africa ianze sijawahi kuona producer anafanya vitu ambavyo navifanya mimi.
"No me si-disrespect mtu am just saying fact na wale producer wa mwanzo wameplay part yao kwa njia waliyoiamini lakini toka hii tasnia ianze toka siku ya kwanza watu wanafanya muziki kwenye production sio generation yoyote hakuna mtu ambaye amefanya vitu nimefanya,”amesema Zombie
Aidha aliendelea kwa kueleza kuwa “Nasimama kwenye hilo kwa sababu nyimbo kubwa mnaziona nikikutajia nyimbo kubwa 10 za Tanzania ambazo zimetrend kimataifa utakuta mimi nina nyimbo zaidi ya saba au sita so unaona kabisa, unaweza kunitajia producer ambaye amefanya nyimbo 50 kwa mwaka au miaka miwili yaani hakuna mtu anayeniweza kwa sababu am the best,”ameeleza Zombie
Mbali na hayo amefunguka kuhusiana na maproducer ambao amewahi kuwafundisha pamoja na nyimbo walizozitoa akiwemo aliyetengeneza wimbo wa ‘Mwakitalema’, aliyetengeneza ‘Salio’, pamoja na Trone ambaye amewahi kufanya ngoma ya ‘Sukari’ ambayo imetazamwa zaidi ya mara milioni 100.
Kwa kipindi cha miaka mitatu mpaka kufikia sasa producer huyo amewahi kutoa ngoma kali zikiwemo Komasava, Ova, Dah, Mapozi, Sensema, Siji, Hakuna Matata, Totorimi, Kunguru na nyinginezo.

Leave a Reply